Tuesday, March 4, 2014

Mzazi afanye haya ili mtoto apate matokeo mazuri

Hivi karibuni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) lilitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne. Kwa mujibu ya matokeo hayo, ufaulu umeongezeka tofauti na mwaka jana. Licha ya malalamiko yanayotolewa na wadau kuwa kilichotangazwa siyo ufaulu halisi, nina mtazamo tofauti kuhusu makundi mawili, yaani waliofaulu na waliofeli. Hatuna budi kuwapongeza waliofaulu na hata shule walizokuwa wakisoma, lakini si sahihi kuwabeza waliofanya vibaya. Kwa wazazi huu ni wakati mwafaka wa kukaa na mtoto kujua kilichotokea. Kwa jumla nataka watu wengi hasa wazazi tujiulize, kwa nini katika mtihani wa aina moja kuwepo na tofauti kubwa ya mtoto anayepata alama zote na mwingine anayekosa alama zote. Kwa nini wanafunzi wanaofundishwa na walimu waliohitimu katika vyuo vya ualimu, watofautiane kimatokeo kama tulivyoona, hasa upande wa shule binafsi na zile za Serikali? Ninaamini upo uwezekano mkubwa wa watoto wote hapa nchini kufaulu kwa alama za juu. Lakini ili dhamira hii itimie yapo mambo muhimu yanayopaswa kupewa kipaumbele: Kwanza wazazi wanatakiwa kujua kipindi cha mitihani mwanafunzi hujenga hofu kubwa, hivyo ni wakati ambao anahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wanaomzunguka. Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatia watoto wao msongo wa mawazo bila kujua, hasa pale wanapobeza juhudi zao. Kwa maana dondoo nne muhimu ambazo naona zinaweza kumsaidia mwanafunzi kufaulu mitihani yake ni kama ifuatavyo: 1. Kuweka mpango madhubuti Kwa kuwa mtihani ni jambo lililo kwenye kalenda ya masomo ya mtoto wako, ni vizuri kuielewa kalenda hiyo na kupanga mipango madhubuti kuhakikisha kuwa mwanafunzi anajiandaa na mitihani mapema. Kuhakikisha mzazi/mlezi unakaa na mwanao na kuangalia vizuri ratiba ya mitihani yake mwezi mmoja kabla ili kuhakikisha anafanya marudio ya masomo yake kuanzia mwanzo.

No comments:

Post a Comment