Monday, March 10, 2014

Video: Nishike mkono - Dknob feat Mwasiti

Queen Darleen na Diamond kuja na ngoma ya pamoja?

Ukikutana tu na picha hizi kwa mara ya kwanza, lazima kitakachokujia kichwani ni collable ya wawili hawa ambao ni ndugu, Queen Darleen na Diamond wameanza kupost picha hizi kupitia katika acc zao za mitandao mbali mbali ya kijamii bila ya kutoa information yoyote juu yake.

Tuesday, March 4, 2014

Nikki Wa Pili atoa tamko: Baada ya habari za kukamatwa kwa tuhuma za wizi Arusha, Weusi wamsimamisha Lord Eyes

Msanii na msemaji mkuu wa Weusi Nikki wa Pili, ametoa tamko juu ya msanii mwenzao Lord Eyes na kusema kuwa kampuni kama kampuni imemsimamisha Lord Eyes na kwa yeyote anaetaka kujua habari zake amtafute Lord mwenyewe. "Tamko ni kwamba Lord Eyes amemsimamishwa kazi, kampuni imemsimisha kazi, kwahiyo kuanzia sasahivi habari zote za Lord Eyes ataziripoti Lord Eyes mwenyew, sababu za kumsimamisha ni za ndani ya kampuni kwahiyo hatuwezi kuzitoa. Kampuni yoyote inamisingi yake ambayo inafanya maamuzi.kwa mamlaka ya kampuni hatuwezi tena kumzungumzia Lord Eyes, kwasasa hivi yeye sio member wa Weusi amesimamishwa mpaka hapo tutakapotangaza upya kumrudisha. Kwahiyo taarifa za Lord Eyes ni zake sio za Weusi tena" amesema Nikki wa Pili

Brand New Single: Jux amuimbia mpenzi wake Jackie Cliff "Nitasubiri"

Chini ya producer Bob Maneck, Jux amefanikiwa kuweka hisia zake kwenye beat na kuzungumza jinsi ambavyo anampenda na jinsi alivyokuwa akijiskia kuwa mbali na mpenzi wake Jacky Cliff mara baada ya madai kuwa alikuwa amekamatwa nchini China . Jux amethibitisha kuwa wimbo huo ni true story inayohusu maisha yake na uhusuniano wake Na Jackie Cliff, ndio maana katika wimbo huu anamuimbia na kumueleza kuwa atasubiri, asilie, asikate tamaa yeye atasubiri ingawa anajua sio mapema lakini atasubiri na atamuona tena. usikilize wimbo huo hapa chini

Mzazi afanye haya ili mtoto apate matokeo mazuri

Hivi karibuni Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) lilitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne. Kwa mujibu ya matokeo hayo, ufaulu umeongezeka tofauti na mwaka jana. Licha ya malalamiko yanayotolewa na wadau kuwa kilichotangazwa siyo ufaulu halisi, nina mtazamo tofauti kuhusu makundi mawili, yaani waliofaulu na waliofeli. Hatuna budi kuwapongeza waliofaulu na hata shule walizokuwa wakisoma, lakini si sahihi kuwabeza waliofanya vibaya. Kwa wazazi huu ni wakati mwafaka wa kukaa na mtoto kujua kilichotokea. Kwa jumla nataka watu wengi hasa wazazi tujiulize, kwa nini katika mtihani wa aina moja kuwepo na tofauti kubwa ya mtoto anayepata alama zote na mwingine anayekosa alama zote. Kwa nini wanafunzi wanaofundishwa na walimu waliohitimu katika vyuo vya ualimu, watofautiane kimatokeo kama tulivyoona, hasa upande wa shule binafsi na zile za Serikali? Ninaamini upo uwezekano mkubwa wa watoto wote hapa nchini kufaulu kwa alama za juu. Lakini ili dhamira hii itimie yapo mambo muhimu yanayopaswa kupewa kipaumbele: Kwanza wazazi wanatakiwa kujua kipindi cha mitihani mwanafunzi hujenga hofu kubwa, hivyo ni wakati ambao anahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wanaomzunguka. Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatia watoto wao msongo wa mawazo bila kujua, hasa pale wanapobeza juhudi zao. Kwa maana dondoo nne muhimu ambazo naona zinaweza kumsaidia mwanafunzi kufaulu mitihani yake ni kama ifuatavyo: 1. Kuweka mpango madhubuti Kwa kuwa mtihani ni jambo lililo kwenye kalenda ya masomo ya mtoto wako, ni vizuri kuielewa kalenda hiyo na kupanga mipango madhubuti kuhakikisha kuwa mwanafunzi anajiandaa na mitihani mapema. Kuhakikisha mzazi/mlezi unakaa na mwanao na kuangalia vizuri ratiba ya mitihani yake mwezi mmoja kabla ili kuhakikisha anafanya marudio ya masomo yake kuanzia mwanzo.

NIMELUDI TENAAAAAAA

ajeeeeeee wadau kama kawa 2014 tupo pamoja. kalibun sana